Uhuru wa mahakama uko wapi?

Ibara ya 107A.-(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema,

“Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Seriikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.”


“Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi”– Rais Samia Hassan Suluhu , Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Hii inathibitisha wazi kuwa mahakama zetu haziko huru, majaji na watumishi wa mahakama wanaongoza kesi kwa kufuata amri za mhimili wa Serikali (Rais), hii ni hatari kubwa sana kwa sababu mahakama ni chombo cha kutenda haki na kusimamia haki za wananchi.

Mara kadhaa Rais amekuwa akizungumzia masuala yaliyopo mahakamani kana kwamba yeye ndiye anayetoa hukumu na kuamua mwenendo wa kazi, yaani akiamuru kesi mbalimbali zisizo na msingi au za kubambikizwa zifutwe au kuendelea, huu sio utaratibu wa kikatiba hata kwa katiba ya sasa imeweka uhuru wa makahama kwa kiasi furani, Kwa kurejea mambo kadhaa yanayoonyesha kwamba kunakuingiwa kwa mahakama ni hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Usa River Mkoani Arusha tarehe 04 Machi, 2023 akiwa katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu siku alisema  “Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi”-Rais Samia Hassan Suluhu  https://www.youtube.com/watch?v=z453XSuveQI

Lakini pia Viongozi wa dini walishawahi kutumia mkutano wao na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumuomba atumie busara kumaliza kesi inayomkabili kiongozi wa Chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake wengine. 

https://www.dw.com/sw/rais-samia-aombwa-kufuta-kesi-ya-mbowe/audio-60997390  lakini pia kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe aliwahi kufanya maombi kama haya, na Rais akajibu huyo mwenzenu kuna makosa amafanya na yatashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, lakini baada ya kelele nyingi za wananchi , Mbowe aliachiwa kwa kile kinachoonekana ni maagizo ya Rais, siku aliyotoka alikwenda Ikulu moja kwa moja usiku wa siku hiyo hiyo, hivyo kuwe mazingira kwamba Rais ameamua kesi yake kutoendelea, kwenye mjadala wa maridhiano pia kuwa mwanachama wa CDM wameachia wakiwa na kesi mbalimbali toka nyakati za uchaguzi 2020, CHADEMA wanasema ni kutokana ma mazungumzo hayo ndio maana wanachama wao wametolewa magerezani, Hii ina maana gani? Pamoja kwamba ni jambo zuri kwa watu wasio na hatia kuachiwa huru, lakini hii inaacha mashaka namna mfumo wa haki inavyoshindwa kuwatendea haki wananchi, na kinachotokea ni kwamba bila fadhila ya rais basi haki zao upotea, hii sio sawa kwa Taifa huru, Taifa ambalo linaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia 

Nini kifanyike…

#KatibaMpya ni suluhisho la uhuru wa mahakama, katiba iliyopo imemapa Rais na mhimili wote wa serikali nguvu ya kuingilia mihimili mingine ikiwemo Bunge na Mahakama, hivyo katiba hii ni hatari kwa maisha ya watanzania wote. Hayati mwalimu Julius Nyerere alishawahi kusema   “Tujenge utamaduni wa kudhibiti viongozi wetu kama wanavunja sheria ya nchi, tusiogope. Mkianza kuwa na woga, nawaambia mtatawaliwa na dikteta. Kama haifanyiki wanadhibitiwa, wale ambao wanavunja Katiba wanadhibitiwa na kusema kweli kabisa lazima tuwe serious katika jambo hilo. Katiba haiwezi kupuuzwa. Akishachaguliwa mtu ataapishwa kuilinda Katiba ili tuweze kumshtaki aliyeikiuka. Mtu yeyote ambaye hawezi kuilinda wala kuisimamia Katiba baada ya kuchaguliwa, hatufai, Udikteta ni Serikali ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache na wao ndiyo huwa sheria. Anayepinga watakayo, basi huonyeshwa cha mtema kuni,”- Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Ni wakati sasa wa kupata katiba mpya ili tujenge nchi kwa misingi ya Demokrasia, sheria na kwa ajili ya wananchi.  

#ChangeTanzaniaLeave a Reply