UBABE WA SERIKALI KUPORA ARDHI YA WANANCHI – KULIKONI?

OVERVIEW

UBABE WA SERIKALI KUPORA ARDHI YA WANANCHI – KULIKONI?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Ardhi ni moja ya nyenzo ya wananchi kujikwamua kiuchumi. Matukio ya wananchi kuporwa ardhi yameongezeka sana hivi karibuni. Wananchi wanashidwa kufanya mikakati yao ya kiuchumi kutokana na kukosa uhakika wa umiliki wa ardhi, serikali imekuwa ikichukua ardhi yao bila kuzingatia sheria za ardhi na haki za kiuchumi. Kuna wananchi wametumia ardhi kwa miaka mingi lakini wanaambiwa waondoke kwa mtazamo tu wa viongozi bila ushahidi wa kisayansi kwa hoja ya kulinda na mazingira, jambo ambalo si sawa. Wananchi wanapata changamoto kubwa sana pale mikakati yao ya uzalishaji chakula kwa ajili ya biashara na matukio yao ya kawaida inapoathiriwa bila kuwazingatia. Kazi ya dola ni kulinda na kuhakikisha kuwa mali ya wananchi inalindwa lakini dola imekaa kimkakati ikisubiri mianya ya kupora ardhi kwa Watanzania, kitu ambacho ni wizi kwa kuwa hakuna uwajibikaji katika katiba yetu.

Adui namba moja wa haki miliki ya ardhi ni katiba yetu, inasema kila mtu ana haki ya kumiliki ardhi lakini katiba hiyo hiyo inasema Rais ndio msimamizi ndio maana anafanya vyovyote anavyotaka. Tunahitaj katibaa ambayo itamfanya Rais pamoja na viongozi wengine wa Serikali wawe na hofu ya kusulubiwa endapo wakifanya makosa. Mfumo wa sasa wa KATIBA umeweka vikwazo vingi sana kwa wananchi kujikomboa kiuchumi kupitia ardhi, kuna maamuzi ya serikali ambayo yanaathiri wananchi katika umiliki wa ardhi hivyo kuleta wasiwasi wa kuendelea ardhi ili kupata mali. Sheria za vijiji zimeshindwa kuheshimika kwa kiwango kikubwa sana. Maamuzi ya Mahakama kuhusu migogoro ya ardhi haiheshimiki na serikali. Tunahitaji #KatibaMpya ili kuongeza haki zaidi kwa wananchi katika umiliki wa ardhi, ardhi ni chanzo kikubwa cha utajiri kwa wananchi. Kupitia umiliki wa ardhi wananchi wanaweza kufanya shughuli za kilimo na ufugaji, kuporwa ardhi kunaondoa kabisa haki yao kiuchumi.  

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchi 

ENGLISH VERSION 

Land is one of the resources that people use to get by economically. Recently there have been several incidents of people being robbed of their land. In turn citizens struggle to make their economic strategies due to the uncertainty of land ownership, the government has been taking citizens land without considering land laws and economic rights. These are citizens who have used their lands for many years but are forcefully evacuated from their lands with a view of conserving the environment without any scientific evidence for such an argument. Citizens experience a great challenge when their food production strategies are affected without their consideration. The government’s job is to ensure that the people’s properties are protected, but the government sits strategically looking for loopholes to loot land from Tanzanians, something that is made possible because there is no accountability in our constitution. 

The number one enemy of land property rights is our constitution, it states that everyone has the right to own land, but the same constitution states that the President is in charge. We need a constitution that will make the President and other government leaders fear for crucifixion if they make mistakes. The current governing system of the constitution has set many obstacles for the people to achieve economic welfare through the use of land. The government has failed to respect village laws to a great extent. Court decisions regarding land disputes are also not respected by the government. We need a new constitution to clearly emphasize the rights of citizens in land ownership. Land is a great source of wealth for citizens, through land ownership citizens can practice agricultural and livestock breeding activities, while the confiscation of land completely denies citizens of these rights.

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchiLeave a Reply