Tozo kila kukicha, ina manufaa au hasara kwa Taifa?

Overview

TOZO KILA KUKICHA, INA MANUFAA AU HASARA YA TAIFA?

MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya  #KataaTozo 

Kwa katiba kodi yeyote inayowekwa ni lazima itungiwe sheria na vinginevyo ni unyanganyi.  Wananchi wamekubali kuwa tozo zilizoongezwa ni hasara kwa taifa kwani wananchi hawaoni huduma zikiboreshwa kwa kodi za hapo awali. Hakuna ubunifu katika kupanua  wigo wa vyanzo vya kodi ila wanaishia kuangalia kitu gani watu wanatumia sana. Kodi zinazoletwa na serikali nyingi ni kwa manufaa yao walio madarakani na marafiki zao. Kodi hizi zimeonekana zikiwawalemea wale ambao hawawezi kujitetea vizuri, yaani wenye kipato cha chini. Mfano mzuri ni kodi iliyo kwenye mafuta ya taa ni kubwa zaidi kuliko iliyo kwenye petrol na dizeli. Na wanaotumia mafuta ya taa ni watanzania wa hali ya chini. Mzigo wa kodi hunawaangukia wananchi wa kipato cha chini. Serikali kuwa na uwezo wa kutoza haimaanishi kuwa inaweza kutoza kodi inavyotaka. Wananchi wapo macho kisiasa na hawakubali  kodi za kipumbavu na wamekubaliana kuwa ni muda wa kuwa na harakati za kisiasa zinazolenga kuibadilisha serikali na sheria za namna hii kwani hazitaisha bila harakati hizi. 

#KataaTozo #ChangeTanzania 

ENGLISH VERSION

Constitutionally, any tax imposed must be accompanied by a law otherwise it is fraud. Tanzanian citizens have agreed that over taxation is disadvantageous to the nation as the fruits of their taxes are not felt nor seen in the services being provided. The government has failed to be innovative in widening the spectrum of tax sources; they instead end up looking at taxing what most people use. Most taxes imposed by the government are seen to be for the benefit of those in power and their friends. These taxes have been seen to burden those who cannot defend themselves well, that is, those with low incomes. A good example is the tax charge on kerosene which is seen to be higher than that on petrol and diesel. And those who use kerosene are low-class Tanzanians. The burden of taxation thus falls on low income citizens. The government having the power to charge taxes does not mean that it can impose taxes as it pleases. Citizens are politically aware and do not accept stupid taxes and together have agreed that it is time to have political movements aimed at changing the government and laws that give room for such things to take place because without it the situation will not end.

#ChangeTanzania



Leave a Reply