Tozo kila kona, Je huduma zimeboreshwa?

This Space features a long and bordering discussion about the volatile nature of the ongoing accumulation of Taxes and Fees that continue to be placed in various sources of money by the government. Citizens continue to complain about the effects of these taxes while many have lamented that the government did not engage its citizens in its plan to introduce these taxes despite the fact that the citizens are the ones who vote to elect the government. Citizens have also seen that there is a need for the government to reduce unnecessary spending in order to reduce expenses rather than increasing exploitative fees on the people.

The discussion explored the effects that come about as a result of the increased imposition of taxes and fees especially on social services like electricity that have more than four different taxes and charges that burden citizens. People have also questioned the government stance that the fees collected are sent to development plans but the development that is being talked about is not seen in the community. 

The discussion also explored the effects of having citizen representatives who side with the government instead of fighting for the rights of the people. This was seen as a major cause of having repressive policies and bills that cannot be questioned anywhere by the representative bodies. Citizens have called upon fellow citizens to cooperate in making their voices heard against the exploitative policies of the government as its effect is felt to not only a few but to all. 

SWAHILI VERSION

Katika SPACE hii kulikuwa na mjadala mrefu na mpana kuhusu utozwaji wa kodi mbalimbali katika vyanzo mbalimbali vya wananchi unaofanywa na serikali. Watu wa matabaka mbalimbali waliendelea kulalamika kutokana na madhara yanayosababishwa na kodi hizo zilizo ongezwa, na walilamaika kutokana na ukweli kwamba hawakushirikishwa katika uundaji wa kodi hizo licha ya kuwa wananchi ndio wanawapatiaserikali mamlaka ya nchi kupitia chaguzi. Pia wannachi walipendekeza kuwa kuna haja ya serikali kupunguza gharama za matumizi ili pesa hizo zifanye masuala ya msingi katika maendeleo kuliko kuendelea kuwanyonya wananchi pasipo faida yoyote.

Madhara ya ongezeko la kodi hizi ni makubwa hususani kwenye huduma za kijamii kama vile umeme ambao mpaka sasa una zaidi ya kodi nne hii inapelekea kuwa kero kubwa kwa wananchi. Lakini watu walihoji pia kwamba serikali inasema kodi wanazokusanya zinakwenda kufanya maendeleo lakini hayo maendeleo hayaonekani katika jamii zetu.

Pia katika space hii watu wamehimiza zaidi uwepo wa ushirikiano baina mwa Watazania wote kwani madhara yatokanayo na sera mbovu za serikali yanawapata watu wote hivyo basi haipaswi kuwaachia watu wachache tu kusema juu yacuovu unaondelea katika jamii zetu. Lakini pia wananchi walisisitiza katika madhara ya kuwa na wawakilishi wao ambao watakaa upande wa serikali badala ya upande wa wananchi kwani hili ndilo suala kubwa linalopelekea hata serikali kupitisha sera na miswada kandamizi ambazo haziwezi kuhojiwa mahala popote na vyombo vya uwakilishi.Leave a Reply