Siasa na Uchumi – Je tunapata Uongozi Tunaostaili.?

OVERVIEW 

SIASA NA UCHUMI – JE TUNAPATA UONGOZI TUNAOSTAHILI?

MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya 

Viongozi ni watatuzi wa matatizo na si vinginevyo lakini sivyo ilivyo katika nchi yetu. Viongozi hawana mawazo ya kujenga nchi bali wanakaa na kufikiria ni wapi pa kumnyonya mwananchi kupitia kodi na tozo. Wananchi wanasema hatuna viongozi tunaostahili kwa sababu hatuna mfumo wa kuwapata. Nchi haina viongozi wenye maono sababu siasa ambayo ndio utawala wa wananchi inaamuliwa na wezi wa kura. Unyonyaji wa kodi umepitiliza nchini. Viongozi wanaongeza tozo bila kujali na kutengeneza nyenzo za wananchi kuongeza vyanzo vya kipato na kukusanyo ya kodi halali bila kuumiza wananchi. Tuna uongozi ambao kiongozi anaweza kumshtaki mwananchi lakini sii mwananchi kumshtaki kiongozi wake. Katiba haituruhusu kuwawajibisha viongozi wetu. Sera mbovu za uchumi zimepelekea mazingira mabovu ya uchumi wa nchi na kusababisha nchi kuendelea kuwa tegemezi. Katiba mpya ni muhimu katika kupata viongozi walio bora na uchumi ulio bora.

#ChangeTanzania 

ENGLISH VERSION

Leaders are problem solvers and not the other way round but that is not the case in our country. Citizens argued that our leaders have no vision with regards to building the country but they keep thinking of ways to exploit the people through taxes and fees. Citizens cited that they do not have the leaders they deserve because we do not have a system to attain such leaders. The country does not have visionary leaders because politics, which governs the people, is built upon stolen votes. Tax exploitation is rampant in the country. Leaders keep increasing taxes instead of creating sources for citizens to increase their sources of income so they can collect legal taxes without hurting citizens. We have a leadership where the leaders can sue citizens but not vice versa. The constitution does not allow us to hold our leaders accountable. Bad economic policies have led to a bad environment for the country’s economy to thrive hence causing the country to continue being dependent. Getting a new constitution is important in order to attain better leaders and a better economy. #ChangeTanzania



Leave a Reply