SAKATA LA BANDARI – TUPANGE HOJA DHIDI YA VIHOJA NA VITISHO.

OVERVIEW   

SAKATA LA BANDARI – TUPANGE HOJA DHIDI YA VIHOJA NA VITISHO

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania   #OkoaBandariZetu  

Sakata la bandari limezua gumzo nchini na Watanzania wengi wametoa maoni yao juu ya suala la mkataba wa bandari. Kutoa maoni na kusikilizwa ni haki ya kila mtanzania kikatiba hasa katika mambo yanayohusu maendeleo ya nchi. Wananchi kupinga mkataba huu ni kutokana na mkataba wenyewe kutokuhusisha wananchi katika hatua za awali lakini pia masharti yaliyoanishwa kwenye mkataba huo kuwa ya kinyonyaji yasiyolenga kuiendeleza Taifa kupitia uwekezaji bali kupoteza rasilimali ya bandari kwenda kwa wageni wa Dubai. Hofu ya wananchi juu ya mkataba huu wa bandari umechangiwa pia na historia mbaya ya kampuni ya DP World katika nchi zilizowahi kuwekeza ikihusishwa na matukio ya rushwa na kuingia mikataba kandamizi. 

Badala ya Serikali kujibu wananchi kwa hoja za msingi imeamua kutumia jeshi la polisi kuwatishia wale wanaopinga mkataba huu ili kushinikiza mkataba huu ukubalike na wananchi. Tumeona aliyekuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dr. Rugemereza Nshala akitishiwa siku chache baada ya kutoa maoni yake juu ya mkataba wa bandari na wananchi wengine kadhaa wameamriwa kuripoti katika vituo vya polisi kujieleza juu ya maoni waliyoyatoa juu ya mkataba huu wa kinyonyaji. Utawala wa vitisho huwa na madhara makubwa mbeleni kwani huweza kupelekea mchafuko katika nchi na kama Taifa hatupaswi kufika huko. muafaka wa kweli kwenye masuala yanayoibua hoja tofuati ni wananchi kusikilizwa na kushirikishwa. Kama hoja za wananchi juu ya uwekezaji wa bandari ungezingatiwa, mjadala huu wa bandari usingekuwa unaendelea. Mjadala huu bado unaendelea sababu sauti za wananchi hazijasikilizwa. Wananchi wananpswa wasikilizwe kwani wao ndio wenye mamlaka ya kweli juu ya rasilimali za nchi yao. 

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchi  #OkoaBandariZetu  

ENGLISH VERSION

The port saga has created a buzz in the country and many Tanzanians have expressed their opinions on the issue. Freedom to freely express oneself and to be heard is a constitutional right of every Tanzanian, especially in matters concerning the development of the country. Citizens are opposing the Tanzanian port contract with DPW because the process did not involve the citizens in the initial stages but also the conditions attached to the contract are exploitative and not aimed at developing the nation through investment but rather aimed at losing the port’s resources to foreigners from Dubai.
The public’s fear concerning the DPW port contract has also been contributed by the bad history of the DP World company in the countries it has invested in to be linked to incidents of corruption and entering into oppressive agreements.

Instead of answering the people with basic arguments, the Government has decided to use the police force to threaten those who oppose this agreement in order to push for this agreement to be accepted by the people. We have seen the former president of the Tanganyika Law Society (TLS) Dr. Rugemereza Nshala being threatened a few days after giving his opinion on the port agreement and several other citizens have been ordered to report to the police stations to give account on the opinions they gave on DPW.
The reign of terror has serious consequences in the future as it can lead to chaos in the country and as a nation we should not get there. The only way to solve this is to give room for the people to be heard and give the corresponding answers based on strong grounds. If the people’s arguments on the DPW contract were considered from their onset, this port debate would not be ongoing. This debate is still ongoing because the voices of the people have not been heard. Citizens should be listened to because they are the sole owners over their country’s resources.

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchiLeave a Reply