Okoa Maisha

ChangeTanzania ilishiriki kikamilifu kwenye kampeni ya #OkoaMaisha kwa kuhamasisha watu kushiriki zoezi la kuchangia damu kupitia mitandao yake yote.

Please visit this link
twitter.com/OkoaMaishaTZ

Kwa Vigezo vya Shirika la Afya duniani, Tanzania inahitaji chupa takriban 450,000 kwa mwaka #OkoaMaishaTZ

Takwimu kimataifa zinaonyesha 8% ya vifo vya akina mama husababishwa na kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua ,

Kaimu Mkurugenzi wa Muhimbili Prof Mseru asisitiza umuhimu wa kuchangia damu wakati wa kutoa huduma ya tiba ya dharura ili ku #OkoaMaishaTz

Uchangiaji damu wa hiari bila malipo na wa mara kwa mara ni msingi wa upatikanaji wa damu salama na ya kutosha” – Prof Museru

Kila mwaka nchi zenye uchumi mkubwa hukusanya damu 15 000 kila kituo, zenye uchumi mdogo hupata chupa 3100 kwa kila kituo. Ktk kipindi cha Jan – Juni 2014, wilaya ya Kinondoni ilikuwa na jumla ya ajali 2,140, Ilala ajali 1,561 na Temeke ajali 1,351

Wachangiaji wa hiari wa damu ni Shujaa waokoaji. Kila siku damu wanayochangia huokoa maelfu ya watanzania. Jiunge nao! Baadhi ya changamoto ni idadi kubwa ya wahitaji damu wa dharura mf akina mama, watoto na majeruhi wa ajali

Usifikiri ukipata ajali, utachangiwa na ndugu yako. Damu itakayokuokoa ni ya mchangiaji hiari.

#OkoaMaishaTz