t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Change Tanzania platform and services:


Rufaa Kesi Ya Wakurugenzi Kusimamia Uchaguzi

Katika kesi ya kupinga Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi iliyokuwa inarindima mahakama ya rufani siku ya leo,  Upande wa serikali wmeweza kuwasilisha hoja kuwa vifungu vile vya sheria ya uchaguzi vipo sahihi na haviondoi uhuru wowote wa tume kama inavyodaiwa na Jopo la mawakili linaloongozwa na Fatma Karume. Mawakili wa serikali katika mahakama ya rufani wamesema kuwa hoja ya wakurugenzi kuwa makada wa vyama vya siasa ni dhaifu kwa kuwa kabla ya uchaguzi huapa viapo vya kuachana na vyama vya siasa.

Zaidi upande wa serikali wamewasilisha hoja kuwa wameamua kukata rufaa kwa kuwa ushahidi uliowasilishwa na Mawakili wa Bob Chacha Wangwe kupeleka picha yenye rangi Nyeusi na Nyeupe  wanapinga na kuiomba mahakama iweze kuondoa ushahidi huo wa picha wa wakurugenzi wanadhaniwa ni makada wa chama tawala kwa kuwa picha zinaweza kutengenezwa.

Jopo la mawakili watano  linaloongizwa na Fatma Karume na Dkt. Shali  wamejibu hoja hizo kuwa suala la kuwepo viapo ni hoja mfu kwa kuwa viapo hivyo havijaelezwa kwenye katiba mama.

 

Fatma Karume na Dkt Shalli wameieleza mahakama kuwa ili Mkurugenzi aseme ameachana na kujiondoa uanachama chama cha  siasa ni lazima kwanza arudishe kadi ya uanachama kitu ambacho huwa hakifanyiki kabla ya kiapo hivyo kusema kula viapo ndio kunathibitisha kuachana na uanachama ni hoja mufu kwa kuwa Wakurugenzi hawajahi wasilisha kadi ya vyama vyao kabla ya kula kiapo. Zaidi Fatma Karume ameiambia mahakama kuwa mtu anaweza kula kiapo na kusema uongo.

 

Jopo la Majaji watano lilikuwepo mahakamani hapo limeahirisha kesi hiyo na itatangaza tena siku nyingine ya kusikiliza kesi hiyo.

 

#ChaguziHuru  #ChangeTanzania


Posted on : 30 July, 2019