t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Change Tanzania platform and services:


Inclusive Development for Citizens Wamkabidhi Spika Wa Bunge Wito Wa Wananchi Uliowekwa Sahihi Na Zaidi Ya Watu 15,000 Kutaka Azimio Kuhusu Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali (Cag

TAARIFA KWA UMMA.

Inclusive Development for Citizens WAMKABIDHI SPIKA WA BUNGE WITO WA WANANCHI ULIOWEKWA SAHIHI NA ZAIDI YA WATU 15,000 KUTAKA AZIMIO KUHUSU MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) LIONDOLEWE.

Jumatatu 8, 2019  

Inclusive Development for Citizens imewasilisha leo rasmi kwa Spika wito wake ulioungwa mkono na wananchi takribani elfu kumi na tano (15,000) inayotaka Bunge liondoe azimio lake la tarehe 02 Aprili ya kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi MKuu wa Hesabu za Serikali. Wito huu ambao upo katika mtandao na sahihi zinawekwa kwa mfumo wa kielektroniki unaendelea kuungwa mkono na kuwekwa sahihi hata baada ya kuwasilishwa. Kilichowasilishwa ni pamoja na majina ya walioweka sahihi pamoja na maoni yao. Wito huu umewasilsihwa kwa njia ya Posta kwenda Ofisi ya Spika Dodoma na pia uliwasilishwa na mkono na wawakilishi katika ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar-es-Salaam

Inclusive Development for Citizens ambayo imekuwa ikiendeleza harakati za raia kupitia mitandao tokea mwaka 2012, imepeleka wito huu na kueleza kuwa njia ya wito (petition) ni njia nzuri, ya kisheria inayotoa fursa kwa wananchi kushinikiza viongozi wao kuhusu kero au suala linalowagusa. Haya yameelezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mbaraka Islam alipoambatana na wawakilishi wengine kupeleka wito huu. “Sisi wananchi tunatimiza wajibu wetu kikatiba na kulinda uwajibikaji na usimamizi wa serikali kama Katiba ilivyoainisha. Mahusiano ya Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu iko kikatiba na si suala la mtu binafsi. Ripoti ya Ukaguzi wa Fedha za Serikali ni lazima zitayarishwe na Profesa Assad ambaye ni Mdhibiti na MKaguzi Mkuu, Bunge lazima lijadili baada ya kuipokea taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Rais ndani ya siku saba (7).” 

Mfumo wa wito (petition) hutumika katika nchi nyingi duniani, mfano Marekani, Ofisi ya Rais (WhiteHouse) ina mfumo huu katika tovuti yake na zikipatikana sahihi laki moja (100,000) basi bila kujali mada, Ofisi ya Rais hushughulikia na kujibu rasmi wito husika. Hapa nchini, Bunge pia lina uwezo wa kujadili maombi  au wito wa wananchi ndani ya Bunge ila inabidi wito huu uwasilishwe na mbunge.

“Inclusive Development for Citizens tunawasihii wabunge wanaounga mkono wito wetu wasimamie ndani ya Bunge na kuwasilisha ombi letu hili, ili liweze kujadiliwa” alisihi na kusisitiza Mratibu wa kitaifa wa Inclusive Development for Citizens, Mshabaha Hamza Mshabaha  na kuongeza  “Katika mfumo wa kidemokrasia, tumefundishwa kuwa serikali ni ya wananchi, kwa ajili ya wananchi, hivyo wabunge waelewe kuwa wananchi tunataka kuona uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma, kama ilivyoainishwa katika Katiba yetu.”

Wito huu kwa Spika na Bunge unaendelea kupokea sahihi kupitia tovuti ya https://www.changetanzania.org/petitions/

Kwa taarifa zaidi wasiliana na Mratibu wa Kitaifa, Mshabaha Hamza Mshabaha +255 22 2198053 barua pepe: mshabaha@changetanzania.org


Posted on : 09 April, 2019