Nchi Kufunguka Na Hali Halisi Kiuchumi.

OVERVIEW 


NCHI KUFUNGUKA NA HALI HALISI KIUCHUMI

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya

Wananchi wamesema kuwa nchi imefunguka kwa kubagua matabaka kwani kiuchumi wengi wao wanaona maisha yao bado ni magumu sana hakuna nafuuu yoyote, Kama uchumi wa  Tanzania umefunguka basi ni kwa watu maalumu hasa walio na fursa ya kujuanza na viongozi au mahusiano ya moja kwa moja na serikali au chama tawala, Kuna ahadi zinasemwa  kuhusu jitihada za kuboresha mazingira ya uwekezaji wa wageni hivyo kwa upande wa miradi ya Kitaifa wawekezaji  kuwa nchi imefunguka, Wananchi wanahoji ni miradi gani hiyo inayoweza kusemwa kwamba imekuja ni ishara ya kufungua nchi,
Wananchi wanasema kufungua kwa usawia lazima kuwe na mababdiliko ya sheria ambayo yatapalilia mazingira bora yenye haki na usawa kwa wakezaji, hii inaweza fanyika kwa kubadilisha mfumo wa sasa wa sheria na katiba, wananchi wanaamini bila kuletwa kwa #KatibaMpya sio rahisi kupata wawekezaji ambao ni makini wenye miradi mikubwa na ya muda mrefu kwa sababu, kufunguka nchi kunakosemwa ni kwa kauli tu na sio mabadiliko ya sheria,
lakini kwa wananchi wa kawaida pia wanasema nchi bado haijafunguka kwani mazingira sio rafiki kwao. Kipindi cha nyuma tuliambiwa kuwa uchumi umekua lakini kwa mtanzania wa kawaida mambo bado hayakubadilika. Pamoja na mfumuko wa bei kutokea hakuna jitihada zimefanyika na Serikali kusaidia wananchi wake,  wafanyakazi bado wanapambana na mfumuko wa bei na mishahara ambayo haijaongezeka  miaka na miaka. Hali ya uchumi kwa watanzania sio nzuri hivyo kwani hata upatikanaji wa mahitaji ya muhimu umekua ni mgumu. Nguvu ya ununuzi ya watu imeshuka.  

#ChangeTanzania 

ENGLISH VERSION

Tanzanians have stated that the country has opened up economically in  discriminative manners, only the elite connected to the  classes rulling party and government official, are benefiting with this called  economic rebuilding stragety ,  there is intangible promises that Tanzania is doing efforts to improve the environment for foreign investment hence in terms of investments on national projects investors will say that the country has opened up but for ordinary citizens the country has not yet producing economic benefits  up because the environment is yet to be friendly to them. In the past we were told that the economy has grown but for the common Tanzanian things did not change on ground. Despite the high level of inflation, no effort has been made by the Government to help its citizens, workers are still fighting inflation and wages that have not increased for years. The economic situation for Tanzanians is not good as citizens stated that even the attainment of essential needs has become difficult. People’s purchasing power has declined.  

#ChangeTanzania Leave a Reply