MIKATABA 36 YA DUBAI EXPO – YALIYOMO NA UHURU WETU 

OVERVIEW  

MIKATABA 36 YA DUBAI EXPO – YALIYOMO NA UHURU WETU 

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Baada ya Rais Samia kuhudhuria maonyesho ya Dubai Maarufu kama Dubai Expo 2020 Februari mwaka jana, mikataba mbalimbali ilisainiwa kati ya nchi hizi mbili. Kati ya mikataba iliyosiniwa ni katika maeneo ya madini, nishati, bandari, na huduma za kidijitali. Moja kati ya mikataba hiyo ni mkataba wa bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World kutoka Dubai. Mkataba huu umezua gumzo katika jamii ya watanzania kwa kuwa ni mkataba mbovu unaouza haki za raia wa kitanzania kwenye umiliki wa rasilimali zao na kuwapa nguvu taifa la kigeni Dubai juu ya rasilimali za nchi. Watanzania wanatambua kuwa uhuru kamili wa nchi ni uhuru wa kiuchumi ambao utapatikana endapo tutajitahidi kutumia rasilimali zetu wenyewe kwa kuwa mikataba inayosainiwa na wawekezaji faida inayopatikana inaenda kwao wawekezaji na nchi yetu inabaki patupu. Kwa kutambua hili, watanzania wanaitaka Serikali iangalie ni kwa namna gani nchi yetu itafaidika na mikataba hiyo bila kuwa watumwa wa wageni. 

Ndani ya miaka 60 ya uhuru kama taifa tumeshindwa kusimamia rasilimali zetu. Kutokuwa na katiba imara kumetupelekea ukosefu wa kusimamia uwajibikaji wa viongozi na serikali inasababisha kuwa na viongozi wasio waadilifu katika kutunza na kuendeleza rasilimali za umma. Serikali ilitangaza kukusanya maoni ndani ya katiba mpya ndani ya miaka mitatu, jambo ambalo si sawa kwani maoni ya wananchi yalishakusanywa na Tume ya Warioba. Huu ni mkakati wao ili kupisha mwaka wa uchaguzi upite bila ya kuwa na #KatibaMpya. Kwa sasa wananchi sio sehemu ya nguvu ya dola ndio maana serikali inafanya inachotaka. Hivyo, ni lazima wananchi wakubali kuleta mapinduzi ya umma ili kuleta #KatibaMpya itakayoweza kuwawajibisha viongozi wasio waadilifu.

#ChangeTanzania   

#WenyeNchiWananchi 

ENGLISH VERSION

After President Samia attended Dubai Expo 2020 in February last year, various contracts were signed between the two countries. Among the contracts  signed are in the areas of mining, energy, ports, and digital services. One of the contracts that has leaked to the public is the port contract between Tanzania and the DP World company from Dubai. This agreement has created a buzz in the Tanzanian community because the terms of the contracts are exploitative, selling off the rights of Tanzanian citizens over their own resources to a foreign nation, Dubai. Tanzanians realize that the full independence of the country encompasses having economic independence that will be achieved only if we strive to use our own resources because the investment contracts signed by investors aim at profiting investors and not our country. Recognizing this, Tanzanians want the Government to look into how our country will benefit from these investment contracts without becoming enslaved to foreigners.

Within 60 years of independence as a nation we have failed to manage our resources. Not having a strong constitution has led us to a failure in holding government leaders accountable. The government has recently announced its plan to collect opinions of the people on the new constitution within the next three years, something that is not right because the opinions of the people have already been collected by the Warioba Commission. This is seen as their strategy to let the election year pass without having a new strong constitution at hand. At the moment, the people do not have a say on their own government, that’s why the government does what it wants without regards to the people’s opinions. Therefore, the people must agree to bring about a public revolution in order to bring about a new constitution that will enable us to hold dishonest leaders into account.

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchiLeave a Reply