Lessons from Kenya #KatibaMpya

OVERVIEW 


#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya
LESSONS FROM KENYA #KATIBAMPYA


Uchaguzi sii uhasama bali ni kutekeleza haki ya kidemokrasia. Mjadala huu ulilenga kupata mafunzo juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Kenya na jinsi gani Tanzania kama nchi inaweza kubadilika kupitia mafunzo hayo. Baadhi ya mafunzo kutoka uchauzi wa Kenya ni juu ya katiba nzuri ya Kenya ambayo wakenya waliipigania ambayo hairuhusu serikali kuingilia ama kujaribu kubana mawasiliano ya mtandao kipindi cha uchaguzi. Waandishi wa habari wako huru kurusha habari na walionekana kuruhusiwa hata ndani ya vituo vya uchaguzi. Wenzetu wanaweza kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi, kuna uhuru wa kutumia mitandao na vyombo vya habari kupeana taarifa za uchaguzi na pia kuna uhuru wa mahakama. Watanzania walitambua kuwa licha ya Kenya kuwa nchi ya Afrika Mashariki, wamepiga hatua kubwa linapokuja suala la demokrasia yenye ufanisi. Wananchi wamehimizana kupigania mifumo bora ya uchaguzi kwa kuanzia na hitaji la katiba mpya.

ENGLISH VERSION

Elections are not meant to be hostile but an act to simply exercise democratic rights. This discussion aimed to draw and learn from Kenya’s general election and how Tanzania as a country can change and build on such lessons. Some of the lessons learned from the Kenyan election is the importance of a good constitution, one in which the Kenyan people fought for, which does not allow the government to interfere or try to restrict internet communication during the election period. In Kenya journalists are free to broadcast news and the media is the given access it needs to make their work possible such as being allowed inside the polling stations. Our colleagues can go to court to challenge the election results, there is freedom to use the networks and the media to share election information and there is also the independence of the courts. Tanzanians realized that despite Kenya being an East African country, they have made great strides when it comes to effective democracy. Tanzanian citizens took upon it as a challenge to fight for better electoral systems starting with the need for a new constitution

#ChangeTanzania 



Leave a Reply