KWA KUPUUZA MAONI YA WANANCHI, CCM INA MASLAHI GANI NA BANDARI ?

OVERVIEW   

KWA KUPUUZA MAONI YA WANANCHI, CCM INA MASLAHI GANI NA BANDARI ?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania   #OkoaBandariZetu 

Wananchi ndio wasemaji wakuu juu ya rasilimali za nchi, si Rais wala wabunge wala kiongozi yeyote wa Serikali. Katika swala la uwekezaji wa bandari za nchi kwenda kwa DP World wananchi hawakuhusishwa ipasavyo kwani Serikali ilichukua nafasi ya kuamua kwa niaba ya wananchi jambo ambalo si sawa kwani limevunja sheria pamoja na haki za wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya kweli. Baada ya swala la mkataba wa bandari kuvuja kwa umma, wananchi wameupinga mkataba huo kwani haujalenga uwekezaji wenye manufaa ya nchi hii. Watanzania wanaamini katika uwekezaji wenye tija na unaoweza kulisogeza Taifa kutoka hatua moja kwenda nyingine. Lakini mkataba huu wa bandari umeonyesha dalili zote za watu kupokea rushwa ili kuupitisha. Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari, hivyo kupitishwa kwa mkataba mkataba huu, ni sawa na ufujaji wa kodi za wananchi kwani vyote vitakuwa chini ya DP World. 

Tatizo la nchi ni mfumo mbovu ambao unatengeneza vyombo vya dola dhalimu na katili ambavyo vinalinda wezi. Sheria za Rasilimali zimewekwa kudhibiti mikataba mibovu kama huu wa DP World, lakini watawala wanavunja sheria makusudi wakijua sheria hazina meno ya kuwawajibisha, na ili kujihakikishia utawala CCM wanazidi kutunga sheria za kuwapa kinga, na kuvunja sheria waziwazi. Wakati sheria zikiwatawaka watawala na wananchi kulinda rasilimali, watawala wanaongoza kuuza rasilimali. Watu wanakanyaga katiba ambayo wameapa kutoivunja. Tuna uongozi ambao hauna uwajibikaji, huu ni udhaifu mkubwa wa katiba yetu. Wananchi waendelee kukumbushana kuwa kwa kila jambo linalotokea nchini liwe kichocheo cha kudai #KatibaMpya, kwa kuwa haya yanayotokea kwa ajili katiba ya sasa imeweka mwanya wa kutokea. 

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchi   #OkoaBandariZetu  

ENGLISH VERSION

The people have a say on matters concerning their country’s resources, not the President, nor parliamentarians, nor any government leader. On the DP World investment on the country’s ports the people were not involved because the government took an initiative to decide on behalf of the people, something that is not right because it has broken the law and the rights of the people who are the real owners in which  power rests. After the port contract with DPW leaked to the public, Tanzanians have opposed the contract as it is not directed at benefitting this country. Tanzanians believe in productive investments that can move the nation from one stage to another. But this DPW port agreement has only made it clear that people were bribed in order to pass it. Tanzania has made a large investment in the port, so the adoption of this contract is equivalent to the waste of citizens’ taxes as all ports authority and assets will be under DP World.

The biggest problem facing the country is the presence of a corrupt system that creates oppressive and cruel government agencies that protect thieves.Laws governing the country’s resource laws are set to control bad and exploitative contracts like the current contract with DP World, but government leaders deliberately break the law knowing that the law has no enough power to hold them accountable, and to assure themselves the administration CCM has been increasingly enacting laws to give them protection, and allow them to openly break the law. While the laws urge government leaders and citizens to protect resources, government leaders have been in the forefront in selling the country’s resources. Leaders are trampling on the constitution that they have sworn not to break. We have a leadership that lacks accountability, this is a major weakness of our constitution. Citizens should continue to remind each other that everything that happens in the country should be an incentive to demand a new constitution because what is happening is made possible by the weakness in the current constitution. 

#ChangeTanzania  #WenyeNchiWananchi   #OkoaBandariZetuLeave a Reply