#KatibaMpya Jana na Leo – Jenerali Ulimwengu  

Jeshi la polisi ni chombo muhimu sana katika nchi hasa katika kulinda amani, demokrasia na utawala bora, Jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi pale wanapokuwa na hoja ya kuwasilisha kwa wananchi kupitia maandamano, hii ni haki ya msingi sana na imewekwa katika misingi ya sheria zetu yaani Katiba.
Wananchi wana haki ya kufikisha malalamiko au hoja za kwa viongozi, namna ya kuwasilisha hoja hizo inaweza kuwa maandamano ya amani, sheria zetu zinaruhusu namna hii ya hisia au mfumo katika kuwasilisha maoni, lakini tumekuwa na uzoefu tofauti sana sana hasa kutokana na matendo ya jeshi la polisi, wao kazi yao nimekuwa ni kuzuia tu, wamekuwa na akili ya aina moja tu ya kuzuia bila kuangalia umuhimu wa wananchi kuwa na nafasi kuwasilisha malalamiko yao. Kama wananchi watakuwa na fursa ya kuwasilisha malalamiko au maoni yao kwa viongozi, ndivyo pia wataweza kuwa na hali ya kusifia au kupongeza viongozi wao. Haya mambo yanaendena sana na ni muhimu yote kwa pamoja yakaheshimika 

 “Polisi hawana uzoefu wa kuratibu maandamano ya namna yoyote kwa muda wa miaka mitano iwe anapongeza au anakosoa huwezi kupata hiyo nafasi. Hii sio sawa kwa Taifa kuwa na polisi na namna hii. 2016 Magufuli alisema Demokrasia kwake yeye ni kuwajengea watu miundombinu kama  barabara, ili waweze kusafirisha mazao na tukampigia makofi na kweli akaanza kujenga mpaka vitu vingine ambavyo hatujui vinatusaiudia walipa kodi. Magufuli alipiga marufuku vyama vya siasa na alisema wazi kuwa kufikia 2020 hakutokuwa na upinzani Tanzania na kweli 2020 tuliona jinsi ambavyo upinzani uliondolewa

Magufuli alipiga marufuku sio upinzani tu hata shughuli za kisiasa ndani ya chama chake mwenyewe hakuna shughuli za kiasa pale katika ccm zinazoendelea isipokuwa ni shughuli zinzohusika na mambo ya kiserikali na kiutawala tu. Imefika 2015 alipoingia Magufuli anachokita yeye ndio inakuwa sera ya nchi, sera ya chama na sera ya serikali kwa hiyo Magufuli ndio alikuwa anaamua. N aipata hii nguvu kutokana na mapungufu makubwa yaliyoko katika katiba yetu ambayo imempa Rais madaraka makubwa zaidi, Hivyo akitokea mtu mwenye sifa kama za Rais magufuli haya ndio matokea yake.

Rais Magufuli kweli alikuwa ni Rais mbaya na hilo wala sitaki kuomba radhi kwa yeyote yule. Rais Magufuli hakufaa kuwa Rais wa nchi yetu na alitufanyia mambo mabaya sana mpaka leo tunaumia kwa sababu mambo aliyoyaacha, na mpaka leo hakuna aliyeyagusa kuna watu wamekaa nayo tu kama vile wamemeza bangi, wanaogopa kuyasema wazi, ili iwe fundisho kwa wengine.

Kuna watu wanamsifia hasa kwa kusema alikuwa anapambana na rushwa, sas msiniambie kuwa alikuwa anapambana na rushwa kwa sababu mtu anayepambana na rushwa hawezi akazuia magazeti yote lakini pia akazuia bunge ili wannachi wasifahamu yanayoendelea.

Mtu anayepambana na rushwa anahitaji sana msaada wa vyombo vya habari vimsaidie kufichua maovu yote, anahitaji sanaa masaada wa bunge huru la kumpa taarifa nini kinatokea nchini kote, sasa kama yeye alikuwa anapambana na Rushwa kwa nini azuie vyombo ambavyo ni msaada kwake katika mapambano na rushwa?

Wale aliowatuma Magufuli kuzima vyombo vya habari bado wako serikalini na sisi tunawafahamu siwezi kumsahau Dr Abbasi, huyu alichangia kuhakikisha vyombo vya habari havifanyi kazi kabisa. Watu kama hawa hawafai kupewa nafasi za kutuongoza kwa sababu hawana nia njema na nchi yetu isipokuwa wapo kwa ajili ya watawala tu.

Tunasikia za chini chini kuwa CCM wataanzisha machakato wa katiba mpya kwa ukubwa lakini matarajio yao yakiwa sio 2025 sasa watu wa aina hii ukiwaamini wewe unakuwa mjinga. Unakuwa ni mjinga kama ukipingana na kila kitu anachosema mpinzani wako, lakini vilevile unakuwa ni bwege kama kila kitu anachokisema mpinzani wako unakichukulia kama ni ukweli. Tusiwaamini na tuendelee kupambana kuhakikisha tunapata katiba mpya nzuri inayotokana na maoni halali ya Wananchi.

#MariaSpaces #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya Leave a Reply