JE MASLAHI YA VYAMA VYA SIASA NDO YA WANANCHI?

OVERVIEW

JE MASLAHI YA VYAMA VYA SIASA NDO YA WANANCHI?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Maslahi ya vyama vya siasa ni tofauti na maslahi ya wananchi, wapo wanasiasa ambao wanazingita zaidi  kulinda maslahi yao binafsi na  vyama vyao. Ni muda wa vyama vya upinzani kutafakari zaidi maslahi ya wananchi hususani katika kupata Katiba. Maridhiano baina ya serikali a vyama vya siasa nchini ni bure pasipo kushirikisha wananchi kwa sababu wananchi ndio huamua hatma ya nchi. Maridhiano ya kweli ni lazima yaguse maslahi ya wananchi. Serikali haijawahi kuwaamini wananchi ndio maana wanaiba kura hivyo, vyama vya upinzani vinapaswa kuelewa kuwa haviwezi kuaminiwa na CCM pasipo #KatibaMpya.

 CCM wametesa watu wengi kutokana na Katiba dhaifu tuliyo nayo ambayo inampatia Rais madaraka makubwa. Sisi sote ni mashahidi kwa rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba kukwamishwa kwa maslahi ya kisiasa nchini, kwani tungekua na Katiba imara na vyama vya siasa imara, Magufuli asingeweza kufanya ukandamizaji aliokuwa akiufanya. Maridhiano ili yawe na sura ya kitaifa ni lazima yaguse maslahi ya wananchi sio kundi la wanasiasa pekee na yanapaswa kufanywa wazi.  Ili kufanya hivi ni lazima tupate muafaka wa kitaifa kwa kupata katiba iliyo bora. Wanasiasa wanapaswa kutambua mzizi mkuu wa  malengo yao yanapaswa kuwa ni wananchi kwanza ambao ni mzizi wa Katiba. Vyama vya siasa vinavyobeba matarajio ya wananchi vinapaswa kuendelea kuonyesha misimamo ili #KatibaMpya ipatikane. Wananchi wanapaswa kuunga mkono Vyama vya upinzani ambavyo vinapigania maslahi ya kupata #KatibaMpya nchini. Katiba ikiwa imara watu wote watajitoa kwa ajili ya Taifa. 

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchi 

ENGLISH VERSION 

The interests of political parties are different from the interests of the people, there are politicians who are there to protect their personal interests and those of their parties. It is time for the opposition parties to reflect more on the interests of the people, especially in getting a new constitution. Democratic reconciliation in the country is futile without involving the people because the people decide the future of their country. Real reconciliation must touch the interests of the people. The government has never trusted the people, that is why they continue to steal votes. The opposition parties should understand that they cannot be trusted by the ruling party, CCM, without the presence of a new constitution.

 CCM has tortured many people due to the presence of a weak constitution which has given the President great powers. We are all witnesses to Judge Warioba’s draft Constitution being blocked for political interests in the country, because if we had a strong constitution and strong political parties in place, the late President Magufuli would not be able to oppress Tanzanians the way that he did.  Reconciliation in order to have a national aspect must touch the interests of the people and not only a group of politicians and it should be done openly. In order to do this, we must find a national framework for a better constitution. Politicians should realize that the main root of their goals should be the citizens first who are the root of the constitution. Political parties that carry the expectations of the people should continue to show their firm stand in the demand for a new constitution. Citizens should support the opposition parties that are fighting for the interests of getting a new constitution in the country because with the presence of a strong constitution, all people will act in the interests of the Nation.

#ChangeTanzania  #WenyeNchiWananchi Leave a Reply