JE MALIASILI ZIKO SALAMA CHINI YA CCM BILA KATIBA MPYA?

OVERVIEW

JE MALIASILI ZIKO SALAMA CHINI YA CCM BILA KATIBA MPYA?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Kwa hali ya sasa na kwa katiba iliyopo wananchi hawawezi kuona thamani ya rasilimali za nchi maana dhamana ya nchi iko chini ya Rais. Ni kwa sababu hiio tumeona maafa yaliyofanyika katika maeneo ya Loliondo na Ngorongoro. Kama wananchi tumeshuhudia pia maliasili zetu zikiibiwa na kupatikana nje ya nchi. Mfano mzuri ni dhahabu. Tumeona pia serikali ikiwapa makampuni ya nje vibali vya kuwinda katika hifadhi zetu za wanyama. Mfano mzuri ni vibali vilivyotolewa kwa kampuni za nje za Green Mile Safari Ltd na OBC kuwinda kwenye hifadhi zetu za wanyama. 

Viongozi wa sasa si waadilifu na hawafanyi kazi kwa ajili ya manufaa ya wananchi bali kwa kujinufaisha wenyewe. Kwa hali hii maliasili zetu haziwezi kuwa salama. Tunahuitaji katiba itakayo toa mamlaka kwa wananchi na kumfanya kila mtanzania kwa nafasi yake kutambua nafasi zao. Moja ya kazi ya vyama vya siasa kuwajibisha serikali lakini kwa sasa ni kinyume chake. Tumeona mikutano ya hadhara ikithibitiwa. Bunge ambalo ni chombo cha kupitia sheria hakiko huru, Rais akiingilia maamuzi ya mahakama na polisi wakifuata maagizo ya viongozi badala ya katiba. Katiba ya sasa haimuwajibishi Rais hvyo rasilimali haziwi katika mikono salama. 

Ili tuweze kunufaika na mali asili ni lazima tuwe na sheria bora. Katiba yetu ni mbovu na haitekelezi matakwa ya wananchi. Bila katiba mpya mali asili zetu zitaendelea kuporwa. Tunahitaji Katiba itakayo mwongoza Rais na si Rais kuongoza mifumo. Katiba itakayo muwajibisha Rais na kupunguza mamlaka ya Rais. Lazima wananchi wawe tayari kupigania  #KatibaMpya kwani bila  #KatibaMpya si tuu maliasili bali hata wananchi hawako salama. 

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi 

ENGLISH VERSION

In the current situation and with the existing constitution, citizens cannot see the value of the country’s resources because the guarantee of the country is under the President. It is for this reason that we have seen the disastrous events that happened in the areas such as Loliondo and Ngorongoro. As citizens, we have also witnessed our natural resources being stolen and found abroad. A good example is gold. We have also seen the government giving foreign companies permits to hunt in our game reserves. A good example is the permits issued to external companies; Green Mile Safari Ltd and OBC to hunt in our game reserves.

The current leaders are not honest and do not work for the benefit of the people but to fulfill their own interests. In this situation our natural resources cannot be safe. We need a constitution that will give power to the people and make every Tanzanian recognize their position. One of the tasks of political parties is to hold the government accountable, but currently it is the opposite. We have seen public meetings proven. Parliament, which is the body that passes laws, is not independent, the President interfering with court decisions and the police following the orders of leaders instead of the constitution. The current constitution does not hold the President accountable, so the resources are not in safe hands.

In order for us to benefit from natural resources, we must have better laws. Our constitution is corrupt and does not fulfill the wishes of the people. Without a new constitution, our natural resources will continue to be looted. We need a Constitution that will guide the President and not the President to guide the systems. The Constitution that will hold the President accountable and reduce his or her powers. The people must be ready to fight for a new Constitution because without a new constitution not only the natural resources but even the Tanzanian people are not safe.
#ChangeTanzania
#WenyeNchiWananchi



Leave a Reply