HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2023/24.

Makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 yameandaliwa kwa kuzingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwemo: Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26) ambao umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020; Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki 2050; Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063; Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2022 – 2027; makubaliano mengine ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

#ChangeTanzaniaLeave a Reply