t

Gallery

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Change Tanzania platform and services:


Inclusive Development for Citizens WATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI OYSTERBAY, WATOA MISAADA.

Leo Ijumaa Mei 17, 2019 Inclusive Development for Citizens walitembelea shue ya sekondari Oysterbay iliyoko msasani jijini Dar es Salaam. Shule hiii inakabiliwa na changamoyo kadhaa wa kadhaa ikiwemo sakafu kuharibika,  kuwa na makataba ndogo pamoja na silingi bodi kubaribika na bati kuchakaa hivyo kupitisha maji pindi kama hizi za mvua. 

Maria Sarungi,  Mkurugenzi mtendaji wa Inclusive Development for Citizens,  Mratibu wa kitaifa wa Change  Bwana Mshabaha Mshabaha,  Mwenyekiti wa serikali za mitaa bwana Harisson Lukosi  waliambatana na wadau mbalimbali kutembelea shule hiyo na kujionea Changamoto hiyo. 

Mratibu wa Kitaifa wa asasi ya  Inclusive Development for Citizens Mshabaha Mshabaha amesisitiza kuwa jamii ina wajibu wa kujitolea kuchangia shule ili kuboresha mazingira ya wanafunzi. "Shule hii inakabiliwa na changamoto lukuki, ukiangalia hii shule na shule zilizoko vijijini zina changamoto sawa tu,  unaweza kukuta shule za vijijini zikawa bora kuliko shule hii,  tuna jukumu kubwa la kujitolea kuchangia shule hizi, ili watoto wetu wasome mazingira mazuri,  tukiiachia serikali pekee shule hizi zitazidi kuwa katika hali mbaya zaidi." Amesisitiza Mshabaha Mshabaha 

Kauli ya Mshabaha Mshabaha  imeungwa mkono na Mkurugenzi na mwanzilishi wa Inclusive Development for Citizens Maria Sarungi aliyesisitiza kuwa wananchi wakiungana kukarabati shule hiyo kwa kuchangia chochote ili kukarabati shule hiyo. "Wenye nchi ni Wananchi,  hivyo niwaombe Watanzania wote tuwe na desturi ya kutembelea shule zetu tulizosoma ili kubaini matatizo yanayozukumba shule zetu ili watoto wetu wasome kwenye mazingira mazuri. " amesisitiza Maria Sarungi. 

Mwenyekiti wa serikali za mitaa ya Oysterbay bwana Harrison Lukosi,  Makamu mkuu wa shule na mwenyekiti wa bodi ya shule wameungana pamoja kuwashukuru Inclusive Development for Citizens kwa kutoa mifuko 21 ya simenti kwa ajili ya kukarabati shule hiyo.

Kumekuwa dhana kuwa shule zilizo kwenye maeneo ya watu wenye kipato kikubwa zinahudumia watoto wa Tabaka la juu suala ambalo sio sahihi kutokana na changamoto zinazo zikabiri shule hii,  shule hii ya Oysterbay watoto wanaosoma ni wa kawaida sana na inakabiliwa na changamoto nyingi zinatakiwa kutatuliwa ili watoto wetu wasome mazingira mazuri na rafiki. 

Shule hii ya Oysterbay ina historia ndefu sana, ilijengwa kipindi cha mkoloni na kipindi hicho ikiwa kama shule ya msingi na baadaye mwaka 2006 ikabadirishwa kuwa shule ya sekondari.