Fahamu Kuhusu Msingi Wa Madaraka Makubwa Ya Rais Katika Nchi Ya Tanzania.

Tulipoingia kwenye mfumo wa urais mwaka 1962 baada ya kupata uhuru mwaka 1961 , hatukuanza maisha tukiwa na Rais, hata wakati wa mkoloni cheo hiki hakikuwepo kabisa kwenye mfumo wa uongozi nchini, huyu kiumbe ni wa mwaka 1962 sio kiumbe wa uhuru Urais ulikuwa baadaye. Tumeingia katika uhuru madaraka ya serikali yalikua chini ya waziri mkuu anayewajibika kwa Bunge, huyu ndiye alikuwa mkuu wa serikali na mtendaji mkuu katika nchi yetu,. Lakini  Bunge kilikua chombo chenye mamlaka makuu ya nchi na Waziri mkuu alikuwa anafanya kazi kwa imani ya Bunge. Waziri mkuu alikuwa anahojiwa na bunge na mambo yote alitakiwa kupitisha bungeni ili atekeleze, japo lilikuwa ni bunge la chama kimoja lakini kulikuwa na upinzani mkali sana ndani ya bunge hilo.

Bunge lilikua na mamlaka ya kumuondoa waziri mkuu  likikosa imani naye kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani kama ilivyo Uingereza, India, Ujerumani, Israel, Japan, Uholanzi kama zilivyo nchi nyingine zote zilizoendelea isipokuwa Marekani na Ufaransa.

Kwenye masuala yanayohitaji mkuu wa nchi kulikua na Gavana General, tulikuwa bado kwenye himaya ya kiingereza. Huu mfumo wa kibunge ni mfumo wa kiingereza. Kwahiyo tuliingia katika uhuru tukiwa na mfumo huu yaani baada ya Malkia kulikuwa na Gavana Jenerali. Gavana Jenerali alikua mkuu wa nchi asiyekuwa na mamalaka ya kiutendaji, kama alivyo mfalme wa uingereza, Rais wa India, Ujerumani, Israel, Malkia wa nchi yoyote wa Ulaya.

Gavana Jenerali alikuwa  head of state na commander in chief kwa jina tu, Mwenye mamlaka ya kiutendaji alikuwa ni waziri mkuu aliyekuwa chini ya Bunge, na kuwajibika kwa bunge.

Mambo  yalibadilika baada ya kupata uhuru, kwani Miezi miwili baada ya uhuru mwalimu Nyerere akajiuzuru  ambaye ndio aliyekuwa waziri mkuu. #MwlNyerere alipojiuliza historia tunayofundishwwa mashuleni tunaambiwa kwamba ajiuzulu kwenda kuimarisha Tanu. Tanu mwaka 1962 ilikua na miaka 7 tu, na ilikua imeongoza uchaguzi mkuu wa mwaka 1960 sasa TANU ilikua na udhaifu gani wa kumfanya Nyerere ajiuzulu ni propaganda na uongo. Maana TANU ilikuwa imemaliza kushinda uchaguzi haikuwa dhaifu.

Kilichomfanya Nyerere kujiuzulu mapema mwaka 1962 miezi michache kabla ya Uhuru kulikuwa na mgogoro mkubwa bungeni juu ya sheria ya Uraia, sheria hii tuliyonayo msingi wake ni mwaka 1962 na kwenye huo mjadala bungeni kulikua na upinzani mkubwa wa wabunge.  Bunge lilikua na Wanachama 81 wa TANU, isipokuwa mmoja tu Mbunge wa Mbulu ambaye Mwl Nyerere na wenzake hawakumpenda wakakataa kumuingiza kama mgombea akaingia kama mgombea binafsi akashinda. Kwenye mjadala wa sheria ya Uraia, Kulikuwa na Upinzani mkubwa Nyerere alisemwa sana na ilimtisha hiyo sheria kupitishwa. Hivyo  akajiuzulu ili kwenda kuandaa mapinduzi ya kikatiba, ili kwenda kuupindua mfumo wa kikatiba unaoipa Bunge mamlaka makubwa. Serikali ya Tanganyika ikawasilisha white paper baada ya Nyerere kujiuzulu  ili Tanganyika iwe Jamhuri  na Nyerere alikwenda kuifanyia kazi.  Hiyo White Paper (waraka mweupe)  ndiyo ilipendekeza Tanganyika iondokane na mfumo wa Waziri mkuu wa kuwajibika Bungeni na ifate mfumo wa Rais kuwa mkuu kiutendaji. 

 Waraka mweupe ulisema yafuatayo juu ya Rais; waraka ulitengenezwa na Nyerere na alisema hivi,  Kwetu sisi Rais atapewa heshima na hadhi anayopewa chifu  au mfalme au chini ya Jamhuri, Rais kwetu sisi hawezi kutofautishwa na mamlaka aliyokuwa nayo mfalme. Habari ya kutenganisha hadi ya mfalme na madaraka kama ilivyo India au Ujerumani au hizi nchi nyingine hii haifai yani tunataka heshima iwe ya kifalme, madaraka yawe ya kifalme na hadhi iwe ya kifalme hauwezi kuitenganisha yaani kwetu sisi hatuwezi kuyatengenisha. Waingereza wameyatengenisha hadhi na heshima ya mfalme na madaraka aliyonayo kwahiyo sisi tunataka kuunganisha. Maana yake tunataka Rais atakayekuwa na madaraka na heshima kama mfalme. Waraka wa serikali ya Tanganyika mwaka 1962 na ndio unaelezea huyó Rais atakuaje; atakuwa mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu na kiongozi mkuu wa serikali, wateule wote wa vyombo  vya dola watakuwa wateule wa Rais. Waraka wa serikali ya Tanganyika mwaka 1962 unaeleza watu wote walio katika utumishi wa umma wasiokuwa wateule wa Raiss watafanya kazi kwa niaba ya Rais, Tume zote, Majaji na kila mtu aliye katika utumishi wa umma atateuliwa na Rais au atafanya kazi kwa niaba. Waraka wa serikali ya Tanganyika mwaka 1962 unaelezA, Rais atapewa mamlaka ya kinidhamu ya kuamua nani afanye kazi nani aondolewe kazini, atapewa mamlaka ya kuteua wabunge, mamlaka ya kuvunja Bunge ambayo hayakuwepo na kuhutubia bunge wakati wowote. Waraka wa serikali ya Tanganyika mwaka 1962 unaeleza Rais atapitisha miswada ya sheria na kuteua watendaji wakuu wa vyombo vyake ikiwemo bunge na mahakama, mamlaka ya kuamua mpaka mishahara ya wabunge yote hi ni kazi ya Nyerere mwaka 1962. Kulikua na upinzani mikubwa ndani ya Bunge kupitisha waraka mweupe lakini Baadae wakamkubalia sasa tukaingia kwenye Jamhuri. Tumetengeneza katiba toka mwaka 1962, Katiba haikutokea kwa bahati mbaya ni Nyerere alitaka iwe hivyo na alipendekeza na kuetetea uwa haoni tofauti kati ya mfalme na Rais. Badaae alitambua madaraka makubwa aliyokuwa nayo mwaka 1967 akasema hivi “Nina mamlaka ya kuwa dictator akizungumza na gazeti la uingereza la Observer 1967 na mwaka 1978 anazunguzma na BBC akasema vile vile, ukweli ni kwamba aliyataka, aliyatetea na kutengeneza mwenyewe. #MwlNyerere hakuwa mtu wa demokrasia mpaka anaondoka madarakani amekuja kufunguka macho akiwa nje ya ikulu, Nyerere aliweka watu kuzuizini maelfu na maelfu, siku tukiingia madarakani mtajua idadi ya watu wahanga wa utawala wa Nyerere. Lakini pia Nyerere alituunganisha na Zanzibar yeye peke yake, muungano haukutokana na azimio baraza la mawaziri, haukutokana na  Bunge ilikua ni siri, siri yake yeye na wasaidizi wake wachache akiwemo waziri wa usalama wa Taifa Bwana Munaka na mwanasheria wa serikali Bwana Rolland Brown na upande wa Karume alikuwa na yule aliyeambiwa akanyoe ndevu huku nyuma wakasaini mkataba. 

Tumetengenezewa mfumo ambao unamtaka Rais atumie utawala wake anavyotaka na kwa kutumia madaraka hayo akapiga marufuku vyama huru vya wafanyakazi mwaka 1964, Akapiga marufuku vyama huru vya ushirika mwaka 1966, Akapiga marufuku serikali mitaa zilizokuwa huru 1972. Nyerere alitumia madaraka yake ya urais akahamisha watu kwa nguvu (opresheni vijiji) 1973 -77 watu zaidi ya milion 8 asilimia 75 walitolewa kwenye maeneo yao kupelekwa katika maeneo yanayoitwa vijiji vya ujamaa.

Nyerere alitumia madaraka yake ya urais akatuingiza katika uchumi dola 1967 Azimio la Arusha liliamuliwa kwa bunge gani? Kanyang’anya watu mali zao kwasababu ya Azimio la Arusha, akapiga marufuku vyombo huru vya habari mwaka 1968-69. Tukaanzishiwa Uhuru na Daily news za serikali na Radio ni moja tu Radio Tanzania, akapiga marufuku vyama vya siasa mwaka 1964-65, Tukatengenezewa mfumo wa kidikteta ambao tunahangaika nao sasa hivi. Ni mfumo wa kidikteta uliotengenezwa na mwalimu Nyerere mwaka 1962 tusije tukasahau hilo kwa sababu kumekuwa na jitihada nyingi sana za kumfanya kuwa mtakatifu sio tu wa kisiasa hata wa kidini na watakatifu huwa hawasemi vibaya. Ili tuondokane na huu mfumo wa Nyerere inabidi tukabiliane naye kwenye mijadala kama hii. Haya mambo yamejulikana muda mrefu sana mwaka 1990-91 wakati tunajiandaa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ilikua ni njia ya kukataa ile legacy ya Nyerere, Tume ya Nyalali ilipendekeza mambo mengi ikiwemo kuwa na katiba mpya ya kidemokrasia ukisoma ripoti ya Nyalali ilikua na juzuu 2 zile zilikuwa ni ukosoaji wa mfumo wetu wa kisiasa kama ulivyojengeka toka 1962, angalau kwamba toka 1961 ulikua unajulikana rasmi huu mfumo wa urais wa kifalme umetuumiza inabidi tuondokje nao na toka wakati huo tumejifunza mambo mengi sana, sasa haya mambo yote tulkiyojifunza yameelezwa vyema sana na tume ya warioba, ila kuna jitihada nyingi za kutusahaulisha kazi kubwa iliyo fanywa na Warioba. Katika juzuu zake Tume ya Warioba kuna volume kubwa kuhusu utafiti kuhusu mambo masuala mbalimbali ya kikatiba, katika tafiti hizo utafiti wa kwanza unaitwa utafiti kuhusu madaraka ya Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania, hili ndilo la kwanza walianza nalo kwasababu wanajua hili ndilo shina la matatizo ya watanzania, kuhusu maadili ya viongozi na uwajibikaji, Kuna utafiti unauhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar,  na kuna ushauri elekezi juu ya mifumo ya uchaguzi na tume ya uchaguzi haya ndiyo mambo manne makubwa ambayo tumeilifanyia uchunguzi mahususi. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchiLeave a Reply