Bima Ya Afya Kwa Wote

OVERVIEW  

BIMA YA AFYA KWA WOTE

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Serikali imepeleka mswada  bungeni wa bima afya kwa wote lakini muswada huo hausemi kipi kitakua chanzo cha mapato cha mfuko huo. Utawala wa Mwalimu Nyerere uliweza kutoa huduma ya afya bure kwa watanzania wote kwa sababu serikali ilihakikisha kuna uchumi wa kilimo, gharama za afya na elimu zililipwa na mapato ya kilimo biashara kama kahawa, lakini serikali zilizofuata ziliua haya mazao, sasa hivi  tumekuwa na uchumi wa uchuuzi. Ili mipango ya bima ifanye kazi ni lazima kuwe na sera za uchumi zinazotekelezwa ili serikali ipate mapato mengine ili kupunguza mzigo wa mwananchi kuchangia kama vile sera za kuongeza ajira. Sera ya afya ya CCM inasema kuwa kila kijiji kiwe na zahanati lakini mpaka Januari 2020 tulikuwa na zahanati 6,467 na tuna vijiji na mitaa 12,319. Sera hiyo pia inasema kila kata iwe na kituo cha afya na tuna kata 4,263 lakini vituo vya afya vilivyopo ni 1,167 mpaka Januari 2020. Wananchi wanahoji kuwa serikali itawezaje kutoa huduma ya afya kwa wote kama miundombinu hakuna? Watanzania wengi wenye kipato cha kawaida hana uhakikia wa chakula cha siku atawezaje kuchangia swala la afya la kesho? Kwakua hakuna mikakati madhubuti ya kuwezesha utoaji wa huduma hii bure kwa wote mwisho wa siku mzigo utawalemea wananchi kupitia kodi. 

#ChangeTanzania  

ENGLISH VERSION

The government has sent a health insurance bill to the parliament but the bill does not say what will be the source of income for the fund. Mwalimu Nyerere’s administration was able to provide free healthcare to all Tanzanians because the government ensured that there was an agrarian economy from which the income from agricultural exports such as coffee funded health and education costs, but subsequent governments killed these crops, were as we’re now an export dependent economy.

In order for insurance schemes to work, there must be economic policies that are implemented to enable the government to get other sources of income so as to reduce the burden of citizens from having to contribute. Chama Cha Mapinduzi’s (CCM) health policy states that every village should have a health clinic but until January 2020 there were only 6,467 clinics and yet we have 12,319 villages and streets. The policy also states that each ward should have a health center, but until January 2020 we had 4,263 wards but the existing health centers were only 1,167. Citizens question how the government will be able to provide universal health care for all if there is no adequate infrastructure?

Many Tanzanians with low income worry about what they will eat for the day, how will they be able to contribute towards health which is a matter of the future? This move by the government has left the citizens worried that since there are no effective strategies to facilitate the universal health coverage plan then at the end of the day, the burden will be shifted to the citizens through taxation. 

#ChangeTanzania



Leave a Reply