Baadhi Hawajaripoti Kazini Katika Teuzi Za Ukuu Wa Wilaya.

Teuzi za  wakuu wa wilaya zilizofanywa na Rais hii ikitokana na  mamlaka yaliyopo kwenye Katiba ya Jamhuri wa Tanzania 1977, Tanzania ina jumla ya wilaya 139, Katika uteuzi uliofanyika hivi karibuni wanawake 42 waliteuliwa na wanaume 97, asilimia kubwa ya wakuu wa wilaya wakibaki kwenye vituo vyao na baadhi kubalidilishwa vituo, ni asilimia 26% tu ndio wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa kinyume kabisa na matalajio ya wengi hasa kwa hoja iliyokuwa imeenza kwenye halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwamba wanakwenda kufanya mabadiliko makubwa ilikupata timu inayoenda na mabadiliko, lakini tunaona 26% ndio mabadiliko na wengine wakiwa wale wale, katika hiyo asilimia 26% ya walioteuliwa wengi ni vijana wa chama waliokosa nafasi za ubunge au viongozi UVCCM. 

Suala ambalo lilikuwa ni la kushtua kidogo ni namna ambayo Rais alifanya mapinduzi ya uongozi wa juu wa CWT kwa kuwasukuma viongozi wote kwenye teuzi ya ukuu wa wilaya, kitu tunachokiona sasa ni kwamba viongozi hao wa CWT hawakuwa wamehusishwa kwenye mchakato wa kuteuliwa kwao, ni waziri serikali inataka waondoka katika nafasi zao za CWT kwa njia ya mapinduzi kwa kutumia ujanja wa UTEUZI? Kuna wakati Teuzi zimekuwa zikitumiaka kama rushwa au namna ya kunyamazisha watu ambao serikali inaogopa sauti zao kutokana na misimamo yao kwa umma,
Lakini katika TEUZI hizi za wakuu wa wilaya hivi karibuni tumeona baadhi ya watu waliokuwa wamepewa TEUZI kimkakati wakishindwa kutokea kwenye tukio la KIAPO, Kutoapishwa kwa wakuu wa wilaya hao kumekuja na maswali mengi, lakini kukiwa na tukio la mmoja ya wateuliwa Japhet Maganga ambaye ni KATIBA wa CWT, kushikiliwa na polisi na kuhojiwa kwa dakika 50 huko Tanga .

Wateule hasa ambao ni viongozi wa ngazi za juu wa Chama Cha Walimu Tanzania ( CWT ) walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya hawajaripoti vituo vyao vya kazi na hawajaapishwa ili kuanza majukumu yao, Rais wa CWT, Leah Ulaya pamoja na Japhet Maganga ambaye ni katibu wa chama hicho  wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT. Kuna hoja nyingi zinaibuka lakini moja ikiwa ni kwamba nafasi wanazoshirikia sasa wanapokea mishahara mara mbili ya kile wanacholipwa wakuu wa wilaya, lakini hoja ya pili iliwa kwamba dhamana ya madaraka waliyonayo sasa ni kubwa sana kulinganisha na ukuu wa wilaya

Hii inaibua hoja ya madai ya #KatibaMpya kutoka na hizi changamoto zinazoibuka kwenye teuzi, uteuzi unaonekana kutozingatia sifa ya mtu na utayari wa kufanyakazi husika, hii inapelekea viongozi kukosa ufanisi au kwenda kutumia maliasili za umma vibaya na ubadhirifu, ni wajibu wa mamlaka za uteuzi kuzingatia hadhi ya sifa ya mtu na nafasi yake, lakini pia kabla ya mtu kutangazwa ameteuliwa ni muhimu akashirikishwa kwenye mchakato ili awe na utayari ya kuchukua nafasi husika au kukataa, Kwenye #KatibaMpya nafasi hizi za uteuzi wananchi wanapendekeza watu wagombee, lakini pia nafasi zisizo na tija ziongolewe

Lakini pia kubwa na linazozua mashaka ni hili la  mahojiano kati yao na polisi na maafisa wa upelelezi na Japhet ? kulikuwa na ulazima gani wa kumhoji Japhet kama yeye hana nia ya kuchukua nafasi ya Ukuu wa wilaya? Mahojiano ya dakika 50 yalihusu nini hasa kwenye uteuzi wa Japhet?  Japhet alipohojiwa na waaandishi wa habari “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT.” Pia Rais wa chama Bi Leah Ulaya hakutoka kuongea chochote na pia maofisa wa chama hicho hawakuruhusiwa kuongea na chombo chochote cha habari.

https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/dc-mteule-ahojiwa-na-polisi-dakika-50-rais-cwt–4104640

Katika kikao kinachohisiwa kuwa cha siri au kisicho rasmi Rais wa chama cha walimu amesikika akisema kuwa chama hicho kipo kwa kuwa wenye nchi wametaka kiwepo na sio walimu kama inavyotarajiwa, hivyo anajaribu kueleza kuna ubabe wa aina fulani unaendelea serikalini, hii ina maana anasihi Tanzania tunatakiwa kuwa na Taasisi huru kama Taasisi bila kufungana na chama chochote cha siasa.

https://drive.google.com/file/d/1JBv_dtc_LiH3RotEHqjLQcLDVnARMq0u/view?usp=sharing
  • Je hii inajaribu kuashiria kuwa hawako tayari kutumikia wananchi au kuna kitu wanakwepa ambacho wanahisi kitawagharimu baadaye? 
  • Je hii inaweza ikahusishwa na maslahi yao hasa ya kifedha?
  • Je inawezekana kuwa ilikuwa ni namna ya kuwatoa madarakani CWT ili wengine wapate nafasi hizo pia? 

Jambo la kukataa teuzi limeibua mijadala mingi mitandaoni na kwa wananchi walio wengi wao wakijiuliza maswali ,Tanzania hakuna haki za kiuchumi , #UhuruWaKujieleza, uhuru kamili  mtu kuchagua ni kazi gani anataka kufanya? Kuna nini kinaendelea CWT kiasi cha kushambuliwa hivi kwa kutumia uteuzi .

Mjadala mkubwa kuhusu Jambo hili pia linahusishwa na mambo ya kimaslahi zaidi katika suala zima la mishahara kati ya nafasi hizo mbili yaani ukuu wa wilaya na Ukatibu au Urais wa Chama Cha Walimu huku inakadiriwa mshahara wa ukuu wa wilaya ni Tsh million tatu pamoja na marupurupu mengine na ukatibu wa chama hicho unasemekana kuwa ni shillingi  7.8 pia kuna marupurupu mengi ambayo wanaona ni bora kubaki katika nafasi zao. Kitu ambacho wananchi wengi wanasema hata wao wangechukua maamuzi ya kukataa nafasi hizo za ukuu wa wilaya. Lakini pia nafasi hizi za Ukuu wa wilaya zinachukuliwa kama nafasi za makada wa chama, hivyo kuondoa kuaminika kwa viongozi au kwamba muda wote walikuwa wanafanya kazi za chama.

.

Yote hayo yanatokea lakini ukitafuta chimbuko la kadhia yote hiyo ni ukosefu wa katiba bora ambayo watu hawa kama wakuu wa wilaya wanachaguliwa na kutenguliwa na Rais na na sio kuchaguliwa na wananchi. Ingefaa zaidi wananchi kuchagua mtu ambaye wanamuona anafaa kuwatumikia kulingana na vipaumbele vyao.

Ni muhimu Rais apunguziwe madaraka ili kuweka utawala bora.

#KatibaMpya  #ChangeTanzaniaLeave a Reply